AN-NUUR 
Na.182 Ramadhan 1419, Januari 1 - 7, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Kona ya Wacha Mungu

Mavuno yangu yasiwe... 

KABLA ya hali hii niliyonayo sasa nilikuwa mstari wa mbele kuwaita watu kwenye kheri. Wakati huo hali yangu kimaisha haikuwa nzuri kama ilivyo sasa. Nilishirikiana na ndugu zangu kwa wema na ucha Mungu. Wote walinipenda na kunifurahia kwa moyo wangu. 

Mwenendo wangu ulianza kubadilika kidogo kidogo baada ya shilingi na nduguze kupiga hodi mara kwa mara nyumbani. Hatimaye wakazoea nyumbani kwangu wakanishawishi niwanyanyapae wale niliotoka nao mbali. Ukapa na mimi tukawa maadui wasio karibiana. Njaa na mimi tulifikishana njia panda, kila mmoja akenda njia yake. 

Taratibu, rafiki yangu mpenzi Ucha Mungu akaanza kunikimbia, hodi hodi zikawa kero kwangu, nilipogongewa mara nyingine niliweza kukaa kimya ndani mpaka huyo aliyegonga alipoondoka. 

Maskini nafsi yangu! Nilijiona Malkia katika himaya ya kusadikika ndani ya kasri la kupendeza. Nilikuwa Malkia niliyejali kitu kuliko utu. 

Mawaidha kadhaa yalinipitikia lakini hayakuweza kuupinda moyo wangu. Niliyakusanya mema niliyoyatenda nikayarusha jaani! 

Watu wote, wakubwa kwa wadogo niliwaweka kiganjani, hakuna aliyethubutu kunikabili, kuninasihi na kunishawishi. Walijikunja kama jongoo mbele yangu! 

Jamani wapi naelekea, njooni, msinikimbie, haya ndiyo maumbile yangu. Nahitaji ushauri wenu, nahitaji nasaha zenu. Mavuno yangu yasiwe mtihani kwangu na kwenu. Nishikeni bega, nivumilieni kwa kauli zangu za kuudhi na maneno yangu ya karaha. Nisameheni kwa yote. Mwenyezi Mungu anatukumbusha sote: 

"Na ajisalimishaye uso wake kwa Mwenyezi Mungu, na hali yakuwa anawafanyia wema (viumbe wenziwe), bila shaka amekwishakamata fundo lililo madhubuti; na mwisho wa mambo yote ni kwa Mwenyezi Mungu". (31:22) 

 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Kingunge, kweli upo uonevu na dhulma

Wananchi wahoji kuhusu polisi aliyeua Arusha

Matokeo ya Darasa la Saba yacheleweshwa kusherehekea sikukuu ya Krismasi: Wananchi wahoji je, nchi hii ina dini moja tu?

Njaa yaikumba Kilwa

Dondoo za Saikolojia
Na. Abu Halima Sachangwa

Kona ya Wacha Mungu
Mavuno yangu yasiwe...

Jicho la Uzalendo: Bhabhoo! Muungwana huyoo!
Na Sompo wa Kahambwe

Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897)

Mafunzo kuhusu funga ya Ramadhani
Imetayarishwa na Africa Muslims Agency

Marekani ni mtetezi au adui wa haki?: Umoja wa Mataifa upo upande gani?
Na Abu Salim

Dawa ya ukimwi ni mwenendo mwema
Na Habiba Swedi, Arusha

Mwalimu Maif: Mwanamke aliyetumia maisha yake kufundisha Qur'an

Ijue  Madrasa Hudaa Arusha

Wazazi waaswa kutoshabikia maovu

Mzee maarufu afariki Moro

Je, hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? (jibu) 
Na Ally Said

Mapinduzi, Muungano kwa manufaa ya nani?

Fufueni EAMWS - Sheikh Amana
Na Habiba Swedi

Msiitupie lawama serikali - Dk. Omar

Baada ya kuvunjiwa nyumba, kuchomewa vyakula na Serikali: Nzasa sasa wafuturu Maembe
Na Q. Mtaita

Acheni mifumo mibovu, fuateni Qur'an - Sheikh Kilemile

Sayansi na Teknolojia 
[Kuunganisha Kompyuta kwa Kutumia Modem

Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Saumu na lishe ya mama anayenyonyesha] 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita