Akamatwa kwa kusikiliza kanda za mahubiri

Na Mwandishi Wetu

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Suleiman Mohammed mkazi wa Ubungo Kibangu, imedaiwa kuwa alikamatwa na polisi kwa tuhuma za kusikiliza kanda zinazodaiwa kukashifu dini nyingine

Imeripotiwa kuwa kijana huyo ambaye ni mtoto wa Mzee maarufu wa eneo hilo Mzee Mohamed Salum Ndumbiko, alikamatwa nyumbani kwao siku ya Jumatano wiki hii saa tatu asubuhi.

Majirani walioshuhudia tukio hilo walieleza kuwa Polisi walifika nyumba anayoishi kijana huyo huku wakiandamana na mtu aliyedhaniwa kupeleka tuhuma hizo polisi.

Aidha walieleza kuwa mara baada ya askari hao kumhoji kijana huo walikwenda nae hadi kituo kidogo cha polisi na hatimaye kuondoka naye hadi kituo cha Urafiki ambako ilisemekana aliwekwa ndani kwa muda, kuhojiwa kisha akaachiwa.