Wazee wa Mwembe (Same) kwa pamoja wanatoa pole kwa Waislamu wa Mwembechai, waliovamiwa na kupigwa na polisi wakiwa msikitini kwao.
Aidha wazee hao wanatoa ushauri kwa Waislamu wote nchini kuswali kwa unyenyekevu zaidi pamoja na kufanya subira ili kukabiliana na hali ngumu inayowakabili Waislamu hivi leo.
Kwa niaba ya wazee hao, Mzee Iddi Mweta amewataka Waislamu wote kulaani vitendo vya kinyama wanavyofanyiwa Waislamu. Pamoja na salamu hizo, wazee hao wametoa mchango wao wa shilingi 5,000/- na wamesema kwamba wanaandelea kukusanya nyingine. Nao Waislamu wa Masjid Manyema Ruaha ametoa shukurani zao za dhati kwa Waislamu wa Dar es Salaam ambao waliwawakilisha katika mapambano yale na polisi pale Mwembechai.
Waislamu hao wa Masjid Manyema, Ruaha wametoa mchango wao wa shilingi 7,615/- kwa kesi za Mwembechai. Michango iliyopokelewa wiki hii kupitia AN-NUUR ni kama ifuatavyo:-
1. Misikiti minne ya Morogoro Sh. 100,000/-. 2. Wanawake waliokuwa wanaswali Mwembechai shs. 10,150/-. 3. Kijiji cha Mwembe (Same) Shs. 5,000/-. 4. Kidatu Shs. 7,615/-. 5. Msikiti wa Karakata Uwanja wa Ndege (DSM) sh. 10,000/-. 6. Masjid N-NUUR Highway Kurasini Shs. 36,000/-.