Wanausalama wetu vipi?

Kwanza walianza kwa kumuua Jenerali Kombe wakasema walidhani ni jambazi, wakawaua vijana sita huko Arusha, wakamezewa, wakarudi jijini na kuua waislamu wasio na silaha na wengine kuwapa vilema vya maisha wakiwa bado wako hopstalini wakiteseka. Mwandishi Badru Kimwaga anaelezea zaidi katika makala hii.

Walipowaua waliokuwa wakilingania dini ya Mwenyezi Mungu, walisema kuwa walikuwa wanalinda Amani, iliyokuwa imetoweshwa na Waislamu wa SIKITI WA Mwembechai… kama ukweli wa kulinda amani ni kuua raia wasio na silaha…..tukajua huenda watatulia na kujutia makosa yao, viongzi wao na wa serikali waliwasifu kwa vitendo hivyo… hewala….

Sio hivyo tu, huko Kimara nako wakaua mtu mmoja bila sababu za msingi tukajua sasa wameacha na kujifunza na kurejea katika maelekezo ya masomo yao waliyoyapata C.C.P. lakini wapi ni juzi tu, mwingine tena, bila haya wala simile, ameuwawa, kisa… mzembe na mzururaji….

Tunajiuliza hivi hawa ni WANAUSALAMA au WAUAJI. Kwa nini jeshi la POLISI, kupitia watumishi wake wanaua raia bila makosa, tuwaelewe nini, ni walinda usalama kweli hawa… mbona hawailindi zaidi ya kutibua hiyo amani… au wengi hukimbia CCP kwa kuogopa mikikimikiki ya wakuu wao huko jeshini… au wengi ni akina ‘Vihiyo’ katika kulinda amani, wakiwa ni wanausalama…. Tunashindwa kuelewa jamani…..

Hivi kumbe kumiliki silaha… hususan bunduki na kuijua jinsi ya kuitumia ni kuua raia…. Ni wapi tunakwenda Watanzania.,,, ikiwa sisi tunaojitia kupanda majukwaani tukihubiri kuwa Tanzania ni nchi yenye AMANI, ndio kwanza tunauana bila kisa, hatujui kuwa tunajengeana chuki baina ya raia na askari polisi….

Kila mtu hata kama hajatia mguu wake darasani kupata kifuta ujinga, anaelewa nje ndani kuwa jeshi la polisi ni wanaolinda Usalama wa raia na mali zao, sasa wengi tunashindwa kuelewa kama kweli watu hawa ni walinzi wa raia na mali zao na hali wao ndio wakuu wautendaji wa vitendo vya mauaji kwa wasio na hatia…

Walipoua Waislamu, wanaolitaja neno la Allah na kumtukuza Mtume Muhammadi, S.A.W. ,polisi walisema kuwa wanadhabiti vurugu… sawa, maana vurugu si kumtaja ALLAH(S.W.)…. Ndio unyonge wetu waumini tusifadhaike sana…. Walipowatoa roho vijana wale wa Arusha, maelezo yakawa ni kuwa wale walikuwa majambazi… lakini ujambazi hukumu yake ni kifo? Tena bila ya kufikishwa mahakamani…. wa Kimara sijui walisema nini maana hata sasa iliingia kichefuchefu kusikiliza utetezi wao.

Kwa Kombe, walisema walimfananisha na mwizi wa magari… jama nyie … hivi kweli mkurugenzi wa usalama wa taifa…. Mshindwe kumtofautisha na mwizi….

Lakini hili la juzi la kuuliwa kwa kijana ambaye alituhumiwa kuwa ni mzembe na Mzururaji, ilikuwa kubwa kuliko… mtu mzururaji kweli…. Anastahili kuuliwa, kwa kosa gani hasa linalostahili kifo, kama sio lawama kwa jeshi hili.

Hivi kweli mtu asiye na kazi unategemea afanye nini… uzembe na huo uzururaji unatokea wapi…. Basi wote tusio na kazi wala ajira maalumu, tukae na kujifungia majumbani kwa hofu ya kukamatwa na saa nyingine kuuliwa kwa ‘makosa makubwa’, yanayoonekana na baadhi ya polisi huku, wale wanaokwamisha maendeleo ya nchi hii wakiendelea kutesa.

Jambo ambalo lilinitia kinyongo na kujenga chuki si kwa polisi huyo muuaji… bali hata uongozi wa mkoa wa polisi kupitia kamanda wake……..Bwana ….Afande Alfred Gewe, ambaye katika kumtetea kijana wake kwa kosa hilo, alisema kuwa kijana aliyeuwawa alifanya uhalifu mtaa wa Jamhuri na kutishia amani katika mitaa ya posta kwa kutaka kumpora askari silaha, ndipo alipouawa… kweli hii kuna mhalifu anaweza kuwa anafanya fujo, risasi impige mgongoni… mbona (Gewe huwi mkweli….)

Mmh…. Hatukubali kutokana na walioshuhudia kusema kuwa mtu huyo, alikuwa ni mmojawapo wa waliofungwa mashati, na walipotakiwa ‘Rushwa’na watendaji wako ‘wazuri’, yeye akaamua kuingia mitini, katika kelele za kumkamata, askari wako, alichomoka akitoka benki anapolinda na kumtia risasi kijana huyo, sasa tukuelewe vipi… amani gani hii yakuua watu ovyo kama wanyama, au mnafikiri binadamu ni ndege, unawawinda tu na kuwalenga shabaha…..

Hivi huko CCP, wanakoenda kusomea mafunzo ya uaskari polisi, wanajifunza kuwatungua raia wema, kama ndege juu ya mti au wanajifunza jinsi ya kulinda usalama wa raia na mali zao, au huko wao wanaenda tu ilimradi waeleweke wameenda…. Maana hakuna athari zozote zinazotokea kuonyesha walivyojifunza kuilinda Amani.

Polisi wameshindwa kupambana na wauza madawa ya kulevya, majambazi, wezi, wala rushwa makahaba… malaya na wale wote wanaostahili kuwekwa kundi moja la wahalifu na kukimbilia kuwatesa na kuwaua raia wema, ni nini hii katika jeshi letu la polisi.

Wanashindwa kuwadhibiti madereva wanaozidisha abiria na kuwazamisha watu mitoni (No Challeage) wanaoendesha mabasi na magari ya abiria kwa mwendo kasi, wanashindwa kukemea uporaji na vitendo vya kinyamawanaotendewa watoto na wanawake, kwa kubakwa kunajisiwa,kulawitiwa navyote vinavyowafanya wajihisi wanyonge na kukimbilia kuwauwa raia wema, tuwaelewe nini hawa.

Hivi Kamanda Jenerali Omari Mahita, halijui hili… au ndio walewale… kwa nini nidhamu na heshima ya jeshi hili linapunguzwa na kuliaibisha lakini amekaa kimya… ni nani atakayekuwa na imani na polisi, ilhali wao ndio watendaji wakuu wa vitendo vya kihalifu… tunajiuliza kwa herufi kubwa WANAUSALAMA hawa wanausalama akilini mwao kweli….