Poleni ndugu zangu Waislamu, Ibilisi hana rafiki

Na Mwinjilisti Kamara Kusupa

  Yule nyoka wa zamani aitwae Ibilisi ana majina mengi yanayofanana na sifa zake. Baadhi yake ni haya:-

(a) Yule mwovu
(b) Mshawishi
(c) Audanganyaye ulimwengu
(d) Mwizi na muuaji ambaye hajikufanya lingine isipokuwa kuiba,kuua, kuchinja na kuharibu.
(e) Ajiinuaye juu ya kila kinachoitwa Mungu n.k.

Ibilisi ana kwaida ya kumtumia binaadamu kama chombokatika biashara yake ya kueneza ubaya duniani na kila aina ya udhalimu katika maisha ya mwanadamu. Kwenye kitabu cha Nabii Ezekieli, Ibilisi ametajwa kama mchuuzi au mfanyi biashara ambaye alikuwako Edeni kwenye bustani ya Mungu tangu mwanzo, na kwamba amefanya uchuuzi na vizazi vingi.

Ibilisi katika biashara yake ya kuchuuza udhalimu ni lazima amtumie mwanadamu. Lakini kwa bahati mbaya mtu anapokaliwa na ibilisi na kutumika kama chombo cha kutembeza ubaya kwa wanadamu wengine mtu huyo yeye binafsi huwa hajitambui. Hata kama wanadamu wenzake watamwambia kwamba ndugu yetu sasa umekuwa chombo cha ibilisi, umebeba udhalimu wa kutuumiza sisi wanadamu wenzako, bado mtu huyo hawezi kuelewa wala kusikia.

Hata hivyo ibilisi kumgeuza mtu kuwa kama kontena lake na kuchukulia bidhaa yake ya ubaya na udhalimu wa kila namna, haina maana kwamba ibilisi anaweza kumpenda ama kumthamini mtu huyo. La hasha! Bali pamoja na kumtumia, bado ibilisi ataendelea kumtesa kwa mateso mbali mbali kiasi kwamba hata wale wanaomnung’unikia mtu huyo hawawezi kujua kwamba yeye anayewatesa,naye pia anateseka pamoja nao isipokuwa anateseka kwa mateso mengine yaliyo tofuati na mateso yao. Hii ni kwa sababu Ibilisi hana udugu na mwanadamu yeyote, wala ibilisi hana rafiki yeyote. Yeye Ibilsi ni aduia wa kila mtu, adui wa watu wote na maduia kwa wakati wote. Mtu ambaye ibilisi amemkalia atajulikana kwa tabia ya uwongo, wizi, uuaji na uharibifu kwasababu yeye mwenyewe ibilisi alikuwa muuaji tangu mwanzo na hakusimama na kweli maana ukweli na haki ndiyo mwiko wa ibilisi. Vivyohivyo taifa ambalo ibilisi amelikalia na kufanya makao ndaniyake, linaweza kutambuliwa kirahisi kutokana na dalili zifuatazo kudhihirika wazi wazi katika maisha yawatu wake, na dalili hizo ni:-

(a)Ukiukaji wa hali ya juu wa haki za binaadamu
(b)Mauaji ya raia wasio na hatia
(c)Wizi, na
(d)Uharibifu wa kila kinachoonekana chema kwa watu na chenye kuwafaa wanadamu katika ujumla wao.

Makala ya Mohamed Said katika AN-NUUR No. 148 ambayo pia ilitolewa mfululizo na gazeti la Rai, imefunua kwa kiasi kidogo tu operesheni za ibilisi katika nchi hii dhidi ya Waislamu ama kama wenyewe mlivyozoea kuita "hujuma" dhidi ya Waislamu na Uislamu. Awali yayote napenda kumpongeza Mohamed Saidi kwa uandishi wake ambao una mpangilio mzuri wa hoja na mtiririko wa mada. Kusema kweli amejitahidi kuwasilisha picha ya kile alichotaka wasomaji waelewe, lakini hata hivyo dosari ile ile iliyoko kwenye makala nyingi za Mohamed Said pia iko katika makala yake juu ya Marehemu Tewa Saidi Tewa. Katika uandishi wake, Mohamed Said ameonyesha ni hodari wa kuchora picha inayomwonyesha msomaji jinsi Waislamu wa Tanzania walivyoonewa ama walivyohujumiwa kwa njia moja au nyingine lakini Mohamed Saidi huwa hatoi hitimisho. Kwa lugha nyingine naweza kusema makala nyingi za Mohamed Said hazina "conclusion", kwa ajili hiyo mtu yeyote aliye makini anashindwa kumwelewa Mohamed Said anataka lifanyike nini hasa ili mambo yawe mazuri kwa Waislamu! Je anataka Ukristo nao uhujumiwe?.

Je anataka Waislamu walipize kisasi kwa kila neno baya walilofanyiwa? Ama anataka Wakristo nao wadhulumiwe haki zao ili kusawazisha mambo? Namwomba Mohamed Said kwa nia njema kabisa ajitahidi kuonyesha hitimisho katika makala zake ili watu tuweze kumwelewa. Atueleze ana mawazo gani ama ana mapendekezo gani ili kuokoa jahazi.

KUKOSA SHABAHA

Neno jingine ambalo napenda niwaeleze wazi na kwa nia njema nyinyi ndugu zetu Waislamu wenye mtizamo kama unavyowasilishwa na gazeti la AN-NUUR ni kwamba mnapotoka sana mnapofananisha kila neno msiloridhika nalo na Ukristo. Kwa mfano mnapolalamika juu ya Mwislamu kunyimwa elimu, mnawafananisha Waislamu wasiosoma na Wakristo wachache waliosoma lakini hamuwatwai Waislamu wasiosoma mkawafananisha na Wakristo wasiosoma ili muone nani kaonewa zaidi. Wala hamuwatwai Waislamu wasiosoma mkawafananisha na Wapagani ama Makafiri (kama mnavyopenda kuwaita ninyi) ambao hawakusoma ili muone nani kadhulumiwa zaidi, badala yake mnatwaa watu wachache tena kwa majina akina Solomon Eliufoo, Padri Simon Chiwanga, Chediel Mgonja, Thabita Siwale, Nikolas Kuhanga na Jackson Makweta ambao ni sehemu (fraction)ndogo sana katika jamii ya watu milioni 30. Je ina maana kwenu kilicho muhimu ni haki za Waislamu tu, lakini haki za watu wasiokuwa Waislamu kwenu si kitu? Mbona hamsemi juu ya akina Mtonya (wa kuleUgogoni) na akina Ole (wa kule umasaini) walionyimwa elimu? Hao nao si ni viumbe wa Mungu kama walivyo hao wa Bagamoyo na Lindi?

Kama kweli ninyi ni wapenda haki basi piganieni haki za watu wote na siyo haki za Waislamu peke yake kwani huo ni ubinafsi na ubaguzi, vinginevyo kwa gia hiyo mnayokwenda nayo jamii haitawaelewa. Kujifananisha na Wakristokwa kila kitu ni kukosa shabaha kwani dini siyo vyama vya upinzani ama vyama vya ushindani kiasi kwamba kila lifanywalo liwe na lengo la kushindana na mwenzi wake au kutupiana vijembe vya maneno kwani kila dini ina malengo yake ambayo yalikusudiwa kutimizwa tangu awali pasipo kujali kwamba dini nyingine ipo au haipo. Je ni kweli kwamba kama Ukristo usingekuwepo hapa nchini ninyi msingeuhubiri Uislamu?Wala Ukristo naUislamu siyo mtu na mke mwenza, hadi ikawa kwamba malalamiko yote yakafanyiwa rejea kwa mwenzake. Kwa wanawake wawili walioolewa namume mmoja ni kawaida kusikia manung’uniko yakwamba mbona watoto wa mwenzangu wanasomeshwa ng’ambo? Mbona mwenzangu kanunuliwa nguo nzuri kuliko zangu? Ama mbona watoto wa mwenzangu wanapendwa lakini wakwangu wanachukiwa? N.k.

Katika masuala ya imani ni vigumu kuainisha ama kutumia "Equation" ya namna ya hesabu za darasani.

Kuna watu kama Marehemu Mohamed Kisoky ambaye alikuwa mkuu wa mkoa wa Iringa miaka hiyo ya 70, yeye kwa bahati mbaya hakuwa anajua kusoma wala kuandika lakini aliaminiwa hadi kupewa ukuu wa mkoa sifa kuu aliyokuwa nayo ni Uislamu. Sasa ni nani awezaye kuamini kauli za kusema Marehemu Tewa Saidi Tewa awe alifukuzwa kwenye uwaziri kwasababu ya Uislamu na siyo mfarakano wa binafsi kati yake na rais wa wakati huo JuliusNyerere?Kwani Tewa Saidi Tewa ana tofauti gani na waasisi wengine wa TANU ambao Nyerere alikosana nao kama akina Marehemu Oscar Kambona?

Nyerere hakuishia kuwatupa nje akina Tewa Said Tewa na Bibi Titi Mohamed tu lakini pia aliwatupa nje na wengine kuwaweka kizuizini kama vile Kassela Bantu, (Mkatoliki) Christopher Kasanga Tumbo (Mkatoliki) Otin Kambona (Muanglikana), Wilfrem Mwakitwange, Modest Choga, na wengineo walifukuzwa ubunge na pia kunyang’anywa uanachama wa TANU ili wasigombee tena nafasi yoyote ya uongozi. Sasa katika sakata la aina hii udini uko wapi? Nasema wazi kwamba mnapotoka sana kwa kuyaangalia mambo kwa jicho la Uislamu dhidi ya Ukristo kwa sababu yote aliyoyafanya Nyerere haikuwa kwa niaba ya Kanisa wala kwa manufaa ya Wakristo katika ujumla wao. Bali alifanya yote kwa niaba ya ubinafsi wake na kwa nia ya kupambana na upinzani bila kujali upinzani huo unatoka dini gani.

Nyerere hakuishia kwa wanasiasa Waislamu au Wanasiasa Wakristo tu bali kutokana na kuogopa upinzani, Nyerere alivunja taasisi ya uchifu ambayoilikuwa muhimu sana kwa maendeleo ya watu na ustawi wa  amii na kuwaweka ndani machifu kadhaa hasa waliokuwa wasomi na wenye kukubalika na makabila yao. Mwisho wa yote akawaundia wananchi nafasi kama za Wakurugenzi wa Maendeleo wa Mikoa na Wilaya ambao kwa kweli waliishi kama watawala mamluki wasiokuwa na mzigo wala uchungu wowote na maendeleo ya maeneo wanayotawala. Hawa walikuwa viongozi wa mishahara, walichokijali nimaslahi ya binafsi tu. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kama Lindi na Bagamoyo wilaya mlizozitolea mifano kwenye makala zenu zingekuwa na watawala wazawa wa maeneo hayo na wenye uchungu na nchi zao, na wanaowajibika kwa watu wao, sio wanaowajibika kwa rais tu aliyewateua, basi huenda wazawa hao wangehimiza maendeleo au kubuni njia za kuwakomboa watu wao na majanga ya umaskini na kukosa elimu, na kwahiyo yawezekana Wilaya hizo zingekuwa tofauti na zilivyo leo.

Dhana ya kwamba uduni wa maendeleo katika maeneo ya Bagamoyo na Lindi, ama upungufu wa shule za sekondari ni kutokana na hujuma dhidi ya Waislamu ni dhana potofu.

Ndoa ya Kanisa na Ukoloni

Hakuna awezaye kubisha kwamba Ukoloni ulifanya kazi pamoja na Kanisa Katoliki, Kanisa la Anglikani, Kanisa la Kilutheri ama dhehebu lolote lililotoka Ulaya enzi hizo. Hii ni kwasababu ukoloni zamani hizo haukuonekana kama ni dhambi ya udhalimu sawa na walivyoona wapingania uhuru wa Afrika akina Kenyatta, Nkrumah na wengineo bali ukoloni ulionekana ni sawa na wito wa Mungu na Utume wa kuwakomboa watu kutoka "Ushenzini" kwenda nuruni. Kwa mfano mtume katika dini ya Kikristo anajulikana kama "Apostle", neno hili limetokana na neno la Kiyunani "Apostolos" ambalo tafsiri yake ni "The one who is sent to establish a new colony" yaani mtu anayetumwa na mtawala wake kwenda kuanzisha koloni jipya. Wakati mwingine hao mitume au "aspostles" waliweza kupewa jeshi dogo lenye silaha ili kama wenyeji wa nchi iliyokusudiwa kufanywa koloni kama wataleta upinzani, basi kwa kutumia nguvu za kijeshi waweze kuzimishwa.

Sasa Bwana Yesu alichangua neno hili "apostolos"na akawaitia wanafunzi wake kumina wawili maana enzi zake lugha ramsi zilikuwa tatu Kiaramu, Kiyunani, na Kirumi. Kirumi ilikuwa ni lugha ya watawala ilitumika maofsini, Kiyunani ilikuwa lugha ya biashara ilitumika katika mataifa yote ya dunia ya wakati huo, na Kiaramu lugha ambayo Yesu aliitumia kuhubiri injili kwenye maeneo mengi ya Uyahudi. Kwahiyo Yesu kama mtu aliyekuja ulimwenguni kuanzisha utawala wa Mungu, aliwachagua wale kumi na wawili nakuwatuma ulimwenguni kote ili kwenda kuanzisha "makoloni" mapya kwa ajili ya Mungu ndiyo maana aliwapa nguvu na uwezokwa kusema "Tazama nimewapa mamlaka na uwezo wa kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule mwovu wala hakuna kitakachowadhuru (Luka). Ninachotaka kusema hapa ni kwamba "ukoloni" wa Mungu kama ulivyokusudiwa na Bwana Yesu ni tofauti kabisa na "ukoloni"wa Mwingereza, Mreno na Mfaransa,katika Afrika.

Kwa mantiki hiyo kanisa Katoliki la Roma, au Kanisa la Anglikan la Uingereza lisingeweza kumpinga mkoloni wala wakoloni wasingediriki kwa namna yoyote kulibughudhi ama kulivuruga kanisa katika shughuli  ake.

Hivyo Kanisa likaachiwa kutoa hudima za jamii kama vile elimu, ka kujenga mashule na vyuo, na huduma za afya kwa kujenga mahospitali na kuwapa wahusika elimu ya udaktari. Katika Tanzania mikoa ile ambayo Wamishenari walifikia kwanza kabla ya kueneza huduma zao nchi nzima kama vile Kilimanjaro, Kagera na Mbeya ndiyo mikoa yenye shule nyingi, vyuo vingi, na hospitali nyingi na pengine sitakosea nikisema ndiyo mikoa yenye wasomi wengi katika nchi hii. Hii ni kwasababu elimu kwa wakazi wa mikoa hii iliingia miaka 100 iliyopita na sasa limekuwa suala na jukumu la kifamilia.

Katika mikoa mingine bado watuwanaona suala la elimu kwa watoto wao ni jukumu la serikali, ndiyo maana serikali sipotilia mkazo kwamba mtoto wako amefikia umri wa kwenda shule ni lazima aandikishwe, mzazi hampeleki shule.

Tupende tusipende kuna watu ambao elimu kwao imeshaingia hadi kwenye utamaduni wao na mila zao nakwahiyo hawawezi kufanana kabisa na wale wasio na mila na utamaduni wa kusoma. Labda nitoe mfano mdogo ulio hai wa kufafanua kauli yangu nisemapo utamaduni wa kusoma. Chukulia kwa mfano makabila mengi  anchi hii yenye mila na deturi za kutahiri wanawake, jukumu la kumtahiri msichana ni la kifamilia kwahiyo hata serikali ingepiga kelele za kukataza tohara bado akina mama wazee watatahiri mabinti zao japo kwa kuiba na kupigana chenga na serikali.

Je ni kwanini watu wa jinsi hiyo hawataki kuelewa wala kusikia juu ya ujumbe wa madhara ya tohara kwa kina mama? Jibu ni kwamba suala la tohara limekwishaingia katika utamaduni wao na hivyo wangeelewa umuhimu wa kuelimisha/kusomesha msichana kama wanavyoelewa umuhimu wa kutahiri msichana ni wazi kwambakatika mikoa yao kusingekuwa na mwanamke asiyejua kusoma na kuandika wala watu wasingengoja serikali ndio iwajengee mashule na kuyagharamia bali wangejenga shule sawa na "makumbi".

Maendeleo na hali bora ya maisha vinakwenda sambamba na elimu, na kwahiyo ili kusawazisha mambo ni watu kuamka na kuanza kuwekeza kwenye elimu.

Nchi za mashariki ya Asia kama Singapore, Korea, Malaysia na nyinginezo zinazovuma kwa maendeleo ya haraka na ustawi wa uchumi wao, watu wameifanya elimu kama "investment" na matokeo yake wamepiga hatua nyingi mbele pasipo kujali kama wao ni Waislamu kama walivyo Waislamu wa Tanzania na penginepo anayependa kuhakikisha atembelee Malaysia nchi ya Kiislamu akajionee, au aende Nigeria nchi iliyotawaliwa na Mwingereza kama Tanzania aone.

Vunja vunja Nyerere

Vunjavunja ya Nyerere haikuishia kwenye taasisi za Kiislamu tu bali Nyerere kama mtawala aliyekusudia kujipa nguvu nyingi na kuwa juu ya wanainchi wote, alivunja vyama vya wafanyikazi (Tanganyika federation of Labour 1964),na kuwaundia wafanyakazi wa nchi hii taasisi bomu ya NUTA, baadaye JUWATA baadaye OTTU na sasa hata sijui inaitwa nini. Kwa kufanya hivyo Nyerere alipora uhuru wa mfanyakazi na haki zake na papo hapo kuhakikisha hicho chombo cha wafanyakazi kinadhibiti watu badala ya kupigania haki zao. Sasa Je, ni kwanini ninyi msipiganie haki za wafanyakazi badala yake mnapigania haki za Waislamu tu? Ama mnataka tuelewe kwamba kitu kiitwacho haki kinapokuwa nje ya eneo la dini ya Kiislamu basi thamani yake inapungua?

Bomoa bomoa ya Nyerere iliendelea hadi kwa wakulima ambao vyama vyao vya ushirika vilivyoanzishwa toka 1920 walivunjiwa pasipo kuelezwakosa la vyama hivyo ni nini.

Matokeo yake wakulima wakawa kama mayatima, wakazalisha mazao lakini yakakosa mnunuzi,na kutokana na kukosa soko la mazao yao, wakulima wa nchi hii wakawa hawana vyanzo cya fedha na mapato mengine na kwahiyo wakasilimishwa na kubatizwa kwenye umaskini wa kudumu. Sasaje hao wakulima ambao ni  aislamu waishio vijijini, na wafanyakazi wWaislamu, na wafanyibiashara wa Kiislamu ambao kwa njia moja au nyingine waliathrika na rungu la dola ya kikandamizaji ya Julius Nyerere ninyi mnawateteaje? Maana inavyoelekea maonevu yote mnayoyalalamikia dhidi ya Waislamu yamelenga Waislamu wa mijini tu lakini waale Waislamu wanaoteseka pamoja na Walalahoi wengine wa nchi hii mmewafanyakuwa si kitu!

IBADA YA SANAMU NA KIPINDI CHAUKIMYA

Tangu utawala wa Nyerereulipopiga marufuku mfumo wa vyama vingi 1963 na kuifanya nchi kuwa mali ya chama kimoja, haki za wanainchi katika maeneo yote ya maisha yaani kiroho (kiimani au haki za kidini), kiuchumi kisiasa na kijamii zimechezewa na kukanyangwa. Watu waliokuwa madarakani bila kujali kama ni Wakristo, Waislamu au Wakomunisti walilewa madaraka sawa na vijana walewavyo bangi, unga au kinywaji chochote kikali na hivyo kuendesha utawala wa maonevu sawa na yale maonevu yamafarao wa Misri.  Kwajili hiyo si vyema Waislamu mkajibagua na kujiweka mbali na wananchi wengine waliodhulumiwa sawa namlivyodhulumiwa ninyi.

Enzi za mfumo wa Chama kimaoja watu waliporwa uhuru na k