NCHI ya Tanganyika ilipitiwa na wakoloni wa aina tatu; Wareno, Wajerumani na Waingereza. Wote hao walikuja kwa lengo moja tu kutafuta utajiri kwa njia ya biashara ama uzalishaji wa kilimo kwa hila na unyonyaji.
Wareno:
Hawakuwa na athari kubwa sana hao licha ya kutuachia zao la korosho pamoja na maneno katika msamiati wa Kiswahili (leso, gereza na kadhalika).
Wajerumani na Waingereza:
Walifanya biashara ya pembe za tembo na watumwa mpaka soko la biashara ya watumwa lilipokufa wakawa wa kwanza kukomesha utadhani hawakuhusika kumbe wapi.
Hao walileta Ukristo, wakaanzisha shule za hesabu, kusoma na kuandika. Walifanya hivyo ili wafuasi wa Ukristo waweze kusoma maandiko matakatifu na kuwapata makarani wa kodi na manyapara wa mashambani.
Waliwatia Waafrika kasumba za Kizungu na kuwafanya wadharau Uafrika na mambo yake. Kisha kuwatawala kimawazo.
Elimu:
Enzi za mkoloni (hasa Muingereza) kulikuwa na shule za misheni na za serikali ya kikoloni. Wanafunzi waliokuwa wanasoma lazima wawe Wakristo ili wapatikane waenezaji wa Neno.
Katika hali hiyo Muislamu hakuwa na nafasi maana elimu iliyokuwa inatolewa ni mafundisho ya dini zaidi kuliko mengine. Hata hivyo, kulikuwa na Waislamu wachache waliosoma wengine walibadili dini moja kwa moja wengine walibadili kwa muda ili baada ya kumaliza masomo warejee katika Uislamu wao.
Baada ya uhuru:
Idadi ya wasomi kubwa ilikuwa ni Wakristo hiyo inakuja akilini kulingana na mfumo wa elimu ya kikoloni. Walikuwepo Waislamu wachache sana wenye shahada za Chuo Kikuu.
Shule ziliendelea kuwa chini ya Makanisa na serikali lakini nyingi za misheni. Mpaka baada ya Azimio la Arusha ambapo miaka ya 70 shule nyingi zilikuwa za serikali. Shule nyingi za seminari za Kikristo ziliendelea kuwa chini ya misheni.
Hivyo ina maana hata baada ya uhuru wanafunzi wa Kikristo walikuwa na nafasi nyingi zaidi za kusoma. Idadi kubwa ya Waislamu imeanza kusoma miaka ya sabini. Kwa mtazamo huo pia si rahisi wasomi wa pande hizo mbili kulingana kwa idadi. Wakati Waislamu wanaanza kutembea wenzao wanakimbia. Tofauti hiyo bado ipo hadi kesho.
Msimamo:
Historia ina kazi moja ya kumuonesha mtu au jamii inakotoka ili atathmini matatizo na mafanikio ya wakati ule. Hapa tunaona kuwa Muislamu hakuwa na jinsi bali alijikuta katika mfumo wenye kupendelea upande mmoja kwa sababu elimu ililetwa na watu wa upande ule kwa hiyo wangenufaika zaidi wafuasi wao. Historia inatuwezesha sisi kutathmini hapa tulipo tunafanya nini? Tunafanikiwa au tunavurunda? Tukishatathmini maendeleo yetu ya sasa historia inatutaka tufikirie mipango na mikakati ya baadaye kulingana na hali ya sasa.
Historia ya Tanganyika imetuachia makovu makubwa sana. Gazeti letu tukufu limejitahidi sana kuyaonesha makovu hayo. Kwa kipindi chote cha uhai wake gazeti limekuwa likionesha athari za mfumo wa tawala za nyuma kwa Waislamu.
Tunaporejea kutaja makovu yaliyoachwa na mfumo
wa siasa zilizopita na zilizopo ni sawa na kufanya maombolezo. Maombolezo
yana muda wake si vizuri kupoteza muda wetu mwingi kuomboleza. Kufanya
hivyo ni kuitia simanzi nyoyo zetu na tusijue la kufanya. Kinachotakiwa
sasa je Waislamu tufanyeje ili tuondokane na hayo? Tukizingatia kuwa serikali
ina mkono wake.
--
![]()
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |