Lakini nilisema pia kwamba pia nina wajibu wa kuishauri serikali yangu
pale ninapoona inafanya makosa.
Wajibu huu mie ninao.
Nililolisema na ninalisema tena leo ni kwamba serikali imekuwa Insensitive
kwa mambo yanayowahusu
Waislamu na mambo mengine. Na kwa kuwa serikali inakuwa insensitive
Waislamu wanatafsiri ile insensivity
ya serikali kuwa bila shaka serikali haiwapendi.
Siku ile nilitoa mfano wa kuingia Msikitini Polisi wa serikali walikuwa hawana sababu ya kuingia Msikitini.
Lakini lile limetokea na ghasia ambazo serikali yenyewe ili contribute
(ilichangia). Kabla ya siku ile polisi
wamekuwa wakiwakamata Masheikh majumbani kwao kimya kimya.
Kama serikali ingekuwa inataka kumkamata Magezi wangeweza kumkamata Magezi nyumbani kwake.
Lakini serikali katika busara zake iliona Magezi imkamate Msikitini
baada ya swala ya Alasiri pale mahala
pamejaa watu. Huku ikijua kwamba Magezi ana wafuasi wake.
Kwanini isimkamate Magezi asubuhi nyumbani kwake? Kwanini isimkamate
Magezi usiku nyumbani kwake?
Wakaamua kumkamata pale. Kitendo kile ndicho kilicholeta rabsha ya
tarehe 12.
Watu walipozidiwa nguvu wakakimbilia ndani ya Msikiti. Msikiti ule una
wanawake ambao hawakuwahi
kutoka.
Sasa mimi bado narudia kwamba kama serikali ingetaka ingeweza kuuzingira
ule Msikiti wale wangetoka tu. Ni
insensitivity yao ya kusema potelea mbali (kwanza) kwanini wangoje
mpaka saa nane za usiku, wakavunja
mlango ambao mpaka leo haujatengenezwa wakaingia ndani. Walishawakatia
umeme na nini. Wakavunja
Msikiti wakaingia ndani. Na si hivyo tu, wakawakamata, wakawapiga wale
wanawake wakawapiga. Na
wakawamwagia unga ambao unawasha. Mimi nilizungumza na wale wanawake
wanaeleza mambo hayo.
Sasa mimi nasema hilo linaonyesha insensivity ya serikali.
Na imefanya kosa kuwashitaki wale Waislamu wa Mwembechai kwa kusema
Yesu si Mungu. Au kusema Yesu
si mwana wa Mungu au kusema Yesu hakusulubiwa. Imefanya kosa kubwa
kuwashitaki wale. Kwa kusema
maneno ambayo ndiyo anayoyaamini miaka yote. Kila mahali palipo na
Uislamu maneno hayo yapo.
Sasa naambiwa habari ya mahakama. Mimi sisemi habari ya mahakama. Nasema
habari ya serikali. Mahakama
inapelekewa kesi. Sasa kesi ya kusema Yesu si Mungu haikutoka kwenye
mahakama.
Haya yametoka nje, polisi ndio waliomshitaki mtu huyu kwa kusema Yesu
si Mungu. Serikali ambayo haina
dini!
Mwaka 1996 walimamatwa vijana wawili Lushoto. Walikuwa Msikitini wanatoa
mawaidha wakasema Yesu si
Mungu. Wakangojewa nje walipokuwa wanakwenda sokoni wakakamatwa. Wakashitakiwa
kwa kosa, kwa
kashfa ya dini nyingine. Dini gani nyingine?
Kashfa yenyewe ni nini wamesema Yesu si Mungu. Na hivi juzi juzi, mambo ndio hayo hayo.
Sasa mimi nasema serikali inafanya kosa kubwa, serikali isiyokuwa na
dini inafanya kosa kuwashitaki watu
kwa sababu ya imani yao.
Hivi karibuni Muadhama Kadinali Pengo amesema kwenye Kiti Moto ya kwamba
kwa Muislamu kusema Yesu
si Mungu si kashfa. Kwasababu ndio imani yake. Na amesema mimi yaani
yeye Kadinali Pengo naamini ya
kwamba Mtume Muhammad si Mtume wa mwisho. Hivyo ndivyo imani yangu.
Si kashfa kwa dini yoyote.
Si hivyo tu, juzi kwenye gazeti la Dar Leo ... kuna maneno Maaskofu
wamuunga mkono K.K. Hawa ni Maaskofu
wa Kanisa la Protestant, na wao wanasema kwa Muislamu kusema Yesu si
Mungu si kashfa. Na kwa Mkristo
kusema Yesu Mungu si kashfa.
Haya ni maneno ambayo yamesemwa na Mabishops, sasa ikiwa dini yenyewe
inayosemwa ni kashfa ni dini ya
Kikristo, Wakristo wenyewe wanasema si kashfa. Sasa serikali inasema
kashfa kwa dini nyingine, dini gani?
Sasa mimi nilichowaomba mnisaidie siku ile ni kuiomba serikali ifute
count hii. Serikali kusema lakini kesi iko
mahakamani si kweli. Serikali bado ina uwezo wa kwenda mahakamani na
kusema tunafuta count hii.
Kuwashitaki kwasababu wanasema maneno yaliyoko ndani ya Qur’an ndio
kusema serikali inaona Qur’an ni
kitabu cha uchochezi.
Unapomshitaki mtu mahakamani kwa uchochezi kwa kusema maneno yaliyo
ndani ya Qur’an, lazima useme na
kitabu chenyewe ni kitabu cha uchochezi.
Sasa ninachosema mimi kwa bahati mbaya hawa kina Bwana walioshtakiwa
kwa count hii moja wamepata
conviction maana yake, mahakama itakuwa inasema kitabu hiki ni kitabu
cha uchochezi.
Swali langu mimi, serikali itaifungia Qur’an? Serikali wataifungia dini
ya Kiislamu? Huo ndio woga wangu
mimi ... hiki kitabu ni kitabu cha uchochezi inabidi kifungiwe. Hawawezi
kuwaambia Waislamu semeni yote
lakini haya Yesi si Mungu msiseme. Sasa hii ndio hatari ninayoiona
mimi.
Kesi ikiwa mahakamani , pale mwenye uwezo ni hakimu. Lakini hakimu anapima
ushahidi uliokuwa pale. Hawa
watu wasema wanastahili kupata dhamana. Hawa watu wanaumwa, wagonjwa.
Jana gazeti moja limesema
Magezi kadhoofu kabisa. Yule Bwana Kamishna amesema Magezi anatibiwa
jela. Na wengine.
Kuna mzee moja Musa Katembo ana umri wa miaka themanini. Basi hata nyie
watu wa magazeti hamna huruma,
mtu wa miaka themanini! Siku hizi mahakama inasema hata mtu aliyeshitakiwa
kwa kuua anaweza kupata
dhamana. Itakuwa huyu mzee wa miaka themanini, atafanya nini huyu akipata
dhamana.
Sasa mie kuishauri serikali kwamba jamani hawa watu wamekaa zaidi ya
miezi mitatu ndani. Ndani kule kuna
adha wamekuwa wagonjwa. Mmoja kesha kufa.
Sasa kusema aah alikuja ndani mgonjwa. Sasa kwanini msimpeleke hospitali!
Sasa huenda akafa mmoja, mmoja
mmoja na dhana ipo. Dhana ipo kwamba serikali inafurahia hivyo; kwamba
wafe mmoja mmoja. Sasa dhana
can be wrong. Na dhana usiitie kwenye sheria.
Kesi ikiwa mahakamani , pale mwenye uwezo ni hakimu. Lakini hakimu anapima
ushahidi uliokuwa pale. Hawa
watu wasema wanastahili kupata dhamana. Hawa watu wanaumwa, wagonjwa.
Jana gazeti moja limesema
Magezi kadhoofu kabisa. Yule Bwana Kamishna amesema Magezi anatibiwa
jela. Na wengine.
Kuna mzee moja Musa Katembo ana umri wa miaka themanini. Basi hata nyie
watu wa magazeti hamna huruma,
mtu wa miaka themanini! Siku hizi mahakama inasema hata mtu aliyeshitakiwa
kwa kuua anaweza kupata
dhamana. Itakuwa huyu mzee wa miaka themanini, atafanya nini huyu akipata
dhamana.
Sasa mie kuishauri serikali kwamba jamani hawa watu wamekaa zaidi ya
miezi mitatu ndani. Ndani kule kuna
adha wamekuwa wagonjwa. Mmoja kesha kufa.
Sasa kusema aah alikuja ndani mgonjwa. Sasa kwanini msimpeleke hospitali!
Sasa huenda akafa mmoja, mmoja
mmoja na dhana ipo. Dhana ipo kwamba serikali inafurahia hivyo; kwamba
wafe mmoja mmoja. Sasa dhana
can be wrong. Na dhana usiitie kwenye sheria.
Sasa isisemwe maneno ya kwamba mahakama ndio inayowaweka. Si kweli.
Mahakama inaamua baada ya
kuambiwa. Waliokuwa wakipinga dhamana siku zote ni serikali. Sasa wakati
ule walikuwa wazima afadhali,
sasa wagonjwa. Kwahiyo, serikali isibabaishe hapa ikasema oh kesi ipo
mahakamani.
Viongozi wangu baadhi wanasema kuwa mimi natafuta umaarufu. Mimi sitafuti
umaarufu. Mimi maarufu. Mimi
sitafuti umaarufu. Mimi tayari maarufu. Kwahiyo, si kweli kwamba mimi
natafuta umaarufu.
Mimi nimeanza ubunge 1965. Na tokea nimeanza ubunge sijagombea nafasi
yoyote mimi nikashindwa. Yoyote.
Sasa umaarufu unakuaje.
Nimegombea ubunge mara nne nimeshinda mara zote nne. Nimegombea udiwani
mara tatu nimeshinda mara zote
tatu. Nimegombea ubunge juzi juzi, nimeshinda. Nimegombea ujumbe wa
kamati ya siasa ya mkoa juzi juzi
nimeshinda. Sasa umaarufu unakuwaje. Mie sitafuti umaarufu.