Baraza Kuu la Waislamu Tanzania huenda likafikishwa mahakamani kufuatia
taarifa yake kwa vyombo vya
habari inayomshutumu Mhe. Kitwana Kondo kwamba kala shilingi milion
28 za Waislamu
Tuhuma hizo nzito zimetolewa na Msemaji Mkuu wa BAKWATA Bw. Yahya Hussein
wakati akiongea na
waandishi wa habari, kufuatia hatua ya Mh. Kondo kuikosoa Serikali
juu ya mwenendo wake uliodhidi ya
Waislamu
Mheshimiwa Kitwana Kondo amesema kwamba tayari anawasiliana na wakili
wake ili aandae taratibu za
kuipeleka BAKWATA mahakamani ikathibitishe juu ya madai yao ya milioni
28.
Akizungumza na waandishi wa habari Mhe. Kondo alisema kwamba ingekuwa
Bw. Yahya Hussein ametoa
shutuma hizo kama mtu binafsi, asingejali. Lakini maadhali amesema
kama BAKWATA chombo ambacho
anaujua uhusiano wake na Serikali, ni lazima ashitaki.
Akiongea na waandishi wa habari kama Mwenyekiti wa Idara ya Habari ya
BAKWATA, Yahya Hussein
alimtuhumu Mhe. Kitwana Kondo kuzihini sh. Milioni 28 fedha za mfuko
wa Sheikh Kassim Foundation
Akizikanusha tuhuma hizo Mhe. Kondo alieleza kwamba yeye ni mdhamini
tu wa mfuko huo na hajawahi
kushika hata senti moja ya mfuko huo.
Aliwataja viongozi wa mfuko huo kwamba ni Sheikh Ismail Mohamed (Mwenyekiti),
Brigedia Hashim Mbita
(Makamu Mwenyekiti);Idd Simba (MP) ambaye ni katibu Mkuu na Sheikh
Khalifa Hamisi (Naibu Katibu
Mkuu).